Posts

Showing posts from July, 2023

ONYO(DISCLAIMER)

1. Kivuli cha kitambulisho chako(digital copy) siyo sawa na Kitambulisho Halisi(Original). Hivyo kwa kubonyeza hapa chini, unakubali kukitumia kivuli kwa matumizi ya Lazima tu, wakati ukiendelea kufuatilia kitambulisho chako halisi kutoka katika ofisi za NIDA wilayani kwako(mahali ulipojiandikisha) 2. Kwa kubonyeza hapa chini unakubali kuwa unawajibika moja kwa moja na madhara yoyote ya kisheria yatakayotokana na matumizi ya kivuli cha kitambulisho chako. NIMEELEWA NIPATIE KIVULI CHA NIDA YANGU

HIVI KITAMBULISHO CHA NIDA KINA UMUHIMU GANI?

Image
Kabla sijaendelea mbele ngoja kwanza nigune (Mmmmmh!) maana si mchezo,  Kuna rafiki yangu alinyimwa kazi kwa sababu alikosa kitambulisho cha Taifa Mwingine alinyimwa mkopo, kwa sababu kuna kipengele cha kuambatanisha kitambulisho chake cha Taifa au Leseni, yeye hakuwa na vyote. Mwingine naye Ameshindwa kupata scholarship, baada ya kuchelewa kufuatilia kitambulisho chake Na kadhalika! na kadhalika!, Mpaka nikawa ninajiuliza, Haya yamekuwa mambo ya 666 nini? NIDA inahitajika kila kona, kila unapogusa Kama bado somo halijaingia, Tovuti ya NIDA imeandika kuwa, ukiwa na Kitambulisho chako au namba  ya kitambulisho; vitakusaidia kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama wakataja; Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration), Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN), Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA, Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport), Kukata Leseni ya Udereva, Kupata Huduma ya Afya, Kufungua Akaunti ya Benki, Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi...

NINATAKA KUJIANDIKISHA NIDA KWA MARA YA KWANZA

Image
Ili kuingia kwenye kanzidata ya Taifa ya NIDA, fuata hatua zifuatazo; Kwanza kabisa, pakua fomu ya usajili ( BONYEZA HAPA ), print halafu ujaze kwa ukamilifu. Pili ambatanisha kivuli cha Cheti cha kuzaliwa andaa na picha za pasipoti(Passport size) Tatu Toa kivuli cha kitambulisho cha mzazi mmoja wapo Nne ongeza kimojawapo kati ya vitu hivi (chochote utakachokuwa nacho);  cheti cha kuhitimu elimu ya msingi kadi ya kupigia kura leseni ya udereva Utambulisho wa mlipa kodi (TIN Number) cheti cha kidato cha 4 na 6  kadi ya bima ya afya kadi ya uanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii. Tano utaipeleka nyaraka zako kwenye ofisi ya serikali ya mtaa/kitongoji unapoishi kwa ajili ya kuweka saini, muhuri kisha waombe wakupe barua ya utambulisho wa mkazi. Baada ya hapo jiandikishe mtandaoni Au utaipeleka nyaraka zako kwenye ofisi za NIDA zilizopo wilayani kwako kwa ajili ya usajili na uchukuaji wa alama za vidole. NIDA watakuambia usubiri, ili wakufanyie mchakato wa kuingiza taarifa z...

JINSI YA KUPATA NIDA YAKO

Image
HITAJI LAKO NI LIPI KATI YA HAYA? SHIDA YANGU NI COPY,  NAMBA  NINAYO TAYARI  NIMEJISAJILI TAYARI, ILA BADO SIJAPEWA NAMBA SINA NAMBA YA NIDA WALA SIJAWAHI KIJISAJILI NAANZIA WAPI? MMKEZANA NIDA, NIDA! KWANI HIYO NIDA INA UMUHIMU GANI? Kama umekutana na changamoto ya kutakiwa kuwa na Kitambulisho Cha NIDA unapotembelea taasisi mbali mbali, serikali ama binafsi, hauko peke yako. Watu wengi wanakumbana na kisiki hicho Cha kutakiwa kuwa na namba ya NIDA au Kitambulisho kabisa.  Yaani kila ukigeuka huku na kule utaambiwa namba ya NIDA mara copy ya kitambulisho iko wapi, ni shida!. kuanzia Leseni ya biashara Leseni ya udereva Taasisi za mikopo (Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ndo kabisaaa, wanataka na kitambulisho cha mdhamini wako) Mabenki Laini za uwakala Pass ya kusafiria Bado hatujazungumzia biashara za mtandaoni kama Forex, Crypto n.k wote wanataka wakufanyie KYC na ili utoboe lazima ku-upload kitambulisho chako. Kila kona ni jau! Mamlaka ya vitambulisho nchini (NIDA)...

COPY YA KITAMBULISHO CHAKO

Image
Kwa kupata kivuli cha Kitambulisho chako BONYEZA HAPA KUPATA COPY Kwa kupata Soft Copy(NIDA online Copy) kwa ajili ya matumizi ya kiofisi wakati ukiendelea kusubiri hard Copy BONYEZA HAPA KUPATA COPY   YAKO Usiache kutoa Maoni yako  hapa chini!