Kabla sijaendelea mbele ngoja kwanza nigune (Mmmmmh!) maana si mchezo, Kuna rafiki yangu alinyimwa kazi kwa sababu alikosa kitambulisho cha Taifa Mwingine alinyimwa mkopo, kwa sababu kuna kipengele cha kuambatanisha kitambulisho chake cha Taifa au Leseni, yeye hakuwa na vyote. Mwingine naye Ameshindwa kupata scholarship, baada ya kuchelewa kufuatilia kitambulisho chake Na kadhalika! na kadhalika!, Mpaka nikawa ninajiuliza, Haya yamekuwa mambo ya 666 nini? NIDA inahitajika kila kona, kila unapogusa Kama bado somo halijaingia, Tovuti ya NIDA imeandika kuwa, ukiwa na Kitambulisho chako au namba ya kitambulisho; vitakusaidia kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama wakataja; Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration), Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN), Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA, Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport), Kukata Leseni ya Udereva, Kupata Huduma ya Afya, Kufungua Akaunti ya Benki, Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi...
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete